Msalabani
pa mwokozi, hapo niliomba upozi,
Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu.
Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu.
Chorus:
Mwana wa Mungu,
Mwokozi wangu,
Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu.
Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu.
Chini
ya mti msumbufu, niliomba utakatifu,
Alinikomboa kwa damu, Mwana wa Mungu.
Alinikomboa kwa damu, Mwana wa Mungu.
Chorus
Aliniokoa
dhambini, ikawa kunikaa ndani,
Aliponifia mtini, Mwana wa Mungu.
Aliponifia mtini, Mwana wa Mungu.
Chorus
Damu
ya Yesu ya thamani, huniokoa makosani,
Huniendesha wokovuni, Mwana wa Mungu.
Huniendesha wokovuni, Mwana wa Mungu.
Chorus
Hicho
kijito cha gharama, leo jivike kwa kuzama,
Kwake uuone uzima, Mwana wa Mungu.
Kwake uuone uzima, Mwana wa Mungu.
No comments:
Post a Comment