Nimeliguza vazi lako Eloheenu, nayo maisha yangu ukayabadilisha
Nimekujua Hoseenu, tena kanipa uhai bila kulipa
Mie nitaubeba mzigo wako Rabii, kwa kuwa mzigo wako ni mwepesi sana
Nira yako ni laini wee Masiya, natamani nifanane nawe siku zote
Wewe ndiye Mungu
hubadiliki, Rohi Baba yangu nakuabudu
Uaminifu wako hauna kipimo,
nayo matendo yako ninayajua
Nilikuwa mtoto sasa mi ni mzee, sijaona siku moja umenitenga
Nisi wanilinda kama mboni lako, hesabu za nywele yangu waielewa
Chorus
Sasa Ebenezar, jibu langu, pumzi uhai wangu tegemeo langu
Huna mwisho wala huna mwanzo Yahweh, natamani nifanane nawe siku zote
No comments:
Post a Comment