Chorus:
Kesha ukiomba kesha
ukiomba,
Kesha ukiomba kesha
ukiomba
Maana adui naye atafuta walio lala,
Maana adui naye atafuta walio lala,
Ili awaangamize roho
yangu usilale
Majaribu
na shida zimetusonga,
Shetani
ajaribu kutuandama kila wakati
Mwenzangu
tusimame imara kwa wokovu
Tukeshe
tukiomba na yote tutashinda.
Chorus
WaKristo
tu wanyonge, wa mwili na wa roho,
Twamwomba
Mungu wetu usiku na mchana
Atupe
nguvu zake tushinde yule mwovu
Maana
bila yeye sisi hatutaweza
Chorus
Shambani
Gethsemane Yesu aliomba
Baba
kiondoe kikombe cha machozi
Maana
sio mapenzi yangu yatimizwe
Bali
mapenzi Yako Baba yatimizwe
Mungu
kampa nguvu kashinda majaribu
Chorus
Kilio
ninacho mimi ni kwa wale wameokoka
Adui
ameamua kamwe hatatuacha
Aleta
majaribu usiku na mchana
Vijana
nawaomba, wazee na watoto
Tusimame
imara, na yote tutashinda
No comments:
Post a Comment